Nadir Haroub: WanaYanga msijali sana kufungwa, bado tupo kwenye mazoezi.

Nahodha wa timu ya Yanga Nadir Haroub 'Canavarro' amewataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kutopoteza matumaini kutokana na matokeo ambao wameonyesha Katika mechi zao za kirafiki.

 Cannavaro ambayo timu yake ilipoteza Kwa 1-0 Jana dhidi ya Ruvu Shooting amesema bado timu ipo vizuri na wanahitaji tu muda kidogo kuweka mambo yote sawa.

Akizungumza na mtandao huu Haroub ametetea timu hiyo na kusema kuwa timu ipo vizuri na ina uwezo wa kufanya vizuri tatizo ni kuwa bado miili yao haijafunguka Kabisa kutokana na aina ya mazoezi wamekuwa wakiyafanya ya fitness.  

Hakuna Muunganiko

-Bado tupo kwenye mazoezi mwalimu anaangalia pia tuna wachezaji wengi wapya ambao wamesajiliwa kwa hiyo bado hakujawa na ule muunganiko lakini mwalimu analifanyia kazi", amesema Nahodha huyo.

Haroub ameongeza kuwa aina ya mazoezi waliyokuwa wakiyafanya Mkoani Morogoro yalihusisha Sana fitness yao na si uwanjani hata hivyo ameahidi matokeo mazuri Katika mechi zijazo.

Bado tupo kwenye mazoezi

-Bado tupo kwenye mazoezi ya fitness ambayo tulikuwa tunayafanya Morogoro kwa hiyo miili yetu bado haijafunguka lakini tunaahidi tutafanya vizuri na mapungufu yaliyojitokeza mwalimu atayafanyia kazi", amesema Haroub.

Yanga wameanza kambi ya siku 9 visiwani Zanzibar ambapo pia watacheza mchezo wa kirafiki wanatumia mazoezi hayo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaofanyika Agosti 23 mwaka huu pamoja na msimu Mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.