Mbeya City yasitisha mkataba wa kocha Kinnah Phiri.

Klabu Mbeya City 'Wanakomakumwanya' leo hii imevunja mkataba na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mmalawi Kinnah Phiri.

Kuvunjwa kwa mkataba huo kunakuja siku chache toka Phiri agome kukifundisha kikosi cha Mbeya City kwa madai ya malimbikizo ya mshahara, huku Mbeya City wakionekana kutomjali kabisa.

Mpaka sasa Mbeya City imecheza michezo miwili ambayo yote Imeongozwa na Kocha msaidizi Mohammed Kijuso.

Katika michezo hiyo Mbeya City wamekusanya alama 3 baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya Majimaji, na kupoteza dhidi ya Ndanda FC.

Rekodi ya Phiri. 

Phiri alijiunga na City Februari 8, 2016 akitokea klabu ya Free State ya Afrika Kusini na ameiongoza Timu hiyo katika michezo 44, akishinda michezo 12, akifungwa 15 na kutoka sare 17 huku akifunga mabao 47 na kufungwa mabao 54.