CECAFA 2017: Zanzibar yaonya wapinzani yaahidi kuendeleza mashambulizi

Kiungo wa timu ya soka ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', Mohammed 'Banka' Issa, ameipongeza timu hiyo kwa kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya Timu ya Rwanda katika michuano ya CECAFA inayoendelea nchini Kenya. 

 Akizungumza na futaa.co.tz Issa amesema pamoja na ushindi huo kuwaongeza motisha ya kufanya vizuri lakini pia umeonyesha uwezo wao. 

 Hata hivyo amemtaka kocha kuangalia makosa madogo waliyoyafanya ili kujiweka vizuri kutokana na ushindani mkubwa uliopo. 

 -Tumeonyesha kiwango kikubwa ila bado tuna mapungufu madogo ambayo yamejitokeza kwenye mchezo huo nadhani mwalimu ameyaona na ataweza kuyafanyia kabla ya mchezo wetu wa pili", amesema mchezaji huyo wa timu ya Mtibwa Sugar. 

 Issa ambaye alichaguliwa mchezaji bora katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Kenyatta mjini Machakos, amesema nia yao ni kushinda mchezo wabpili ambao utakuea dhidi ya ndugu yao Kilimanjaro Stars Alhamisi.